Akiongea na
Bongo5, HK amesema, “Hata wakiikataa hii script ya pili tutawapelekea script
nyingine.”
“Tumeshapeleka
script nyingine zaidi ya wiki tatu zilizopita na nimewapigia simu jana
wameniambia bado hata kuipitia bado hawajaipitia. Tulikubaliana na serikali
kuwa ni lazima video ya ‘Chura’ ifanyike,” alisema HK.
“Script
tuliyowapelekea ni ya kawaida sana, kama wataikataa itabidi tuziweke zote mbili
hadharani ili watu wachangie kwa kuwa hata ile ya kwanza haikuwa mbaya,
walisema kuwa haina ujumbe kwahiyo kwenye script ya sasa hivi tumezingatia
maamuzi yao waliyoyataka kwenye script hiyo,” ameongeza.
Hivi
karibuni Snura ameachia wimbo wake mpya ‘Shindu’ ambao unazidi kufanya vizuri
kwenye redio na mitaani pia.
ANGALIA VIDEO YA HARMONIZE INAVYOZIDI KUSHIKA KASI NAKUPASUA NCHI JIRANI!
No comments:
Post a Comment