
Familia ya
Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Mvomero mkoani Morogoro, Peter Sinto waliokuwa
wakitokea mkoani Tabora kujitambulisha kwa wazazi wa mwanamume baada ya kufunga
ndoa, ni miongoni mwa watu 31 waliofariki dunia kwenye ajali ya mabasi ya
Kampuni ya City Boy.
Ajali hiyo
iliyohusisha mabasi mawili ya kampuni hiyo, moja likitokea Dar es Salaam
kuelekea Kahama mkoani Shinyanga na lingine likitokea Kahama mkoani Shinyanga
kuelekea Dar es
Salaam.
Tukio hilo
lilitokea saa tisa jana katika eneo la Maweni, Kata ya
Kintiku,
Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.
Akizungumza
leo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Said
Mussa
amesema katika ajali hiyo amempoteza baba yake mdogo Sinto na mkewe Rose na
mtoto wao mdogo.
“Walifunga
harusi mkoani Mbeya ukweni kwa hiyo walikuwa wakitoka kujitambulisha nyumbani
kwa baba mdogo mkoani Tabora,”amesema Mussa.
No comments:
Post a Comment