Mapenzi ya
Diamond Platnumz na Wema Sepetu ni miongoni mwa mapenzi yaliokuwa kwenye midomo
ya Watanzania wengi kutokana na watu wengi kuvutiwa na ‘Couple’ hiyo,mwishoni
mwa mwaka 2014 waliingia kwenye headlines za kuachana na kila mmoja kuendelea
na maisha yake.
Diamond
Platnumz kwa sasa yuko na Mama mtoto wake Zari huku Wema Sepetu akiwa na
mshindi wa Big Brother 2014 Idris Sultan,toka Diamond na Wema Sepetu kuachana
tumesikia mara kadhaa wakiripotiwa kuwa hawaelewani,lakini July 05 Diamond
Platnumz ameamua kuonyeshesha kuwa hawana tofauti kwa kupost tangazo la show ya
Christuan Bella na Idris Sultan show ambayo inasemekana imeandaliwa na Wema
Sepetu.
No comments:
Post a Comment