Filamu hiyo
inaingia sokoni Ijumaa hii kwa mfumo wa dijitali ambapo watu watainunua na
kuingalia kwenye smartphone zao kupitia app ya Proin Box.
Lulu
ameiambia MWAKASEGE BLOG kuwa filamu hiyo imekuja na mapinduzi makubwa kwa kila kitu
kuanzia teknolojia na uigizaji. Amedai kuwa yeye na kampuni yake ya Proin,
walitaka kuja na kitu tofauti na vilivyozoeleka kwenye filamu za Tanzania.
“Ilitubidi
kwa kiasi fulani tutulie, tusome mazingira, tasnia yetu inamiss nini sasa hivi,
mashabiki wetu wanahitaji nini sasa hivi,” anasema Lulu.
“Tumejitahidi
kufanya production ya tofauti ambayo ina quality nzuri, it needs time, sio kama
zamani kwa siku mnaweza mkashoot scene sita, saba, lakini saa zingine
production kwa siku tulikuwa tunaweza kushoot scene mbili tu lakini
mnahakikisha mnatoka na kitu kizuri,” ameongeza.
Amedai kuwa
hata sauti zingine pia ilibidi waziingize upya studio ili kuwa na kitu bora
kama ambavyo hufanyika kwenye filamu za Hollywood.
KAMA ULIPITWA NIMEKUSOGEZEA, WIMBO MPYA WA DIAMOND PLATNUMZ FT P SQUARE UMEVUNJA #RECORD BONYEZA HAPA CHINI KUONA!!
No comments:
Post a Comment