
Kamishna wa
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Simon Sirro amewataka wale wote
waliyo na vyeti vya kugushi (vyeti feki) wajisalimishe mapema kwa jeshi hilo
kabla ya kuanza kwa oparesheni maalum utakaowabaini na kuwachukulia hatua za
kisheria.
Kamanda
Sirro ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar
na kuongeza kuwa, watuhumiwa wamekuwa wakibanwa na kuwataja baadhi ya vigogo wa
seriaklini kuwa ndiyo wanaohusika kuwatengenezea vyeti hivyo na kwamba
huvitumia vyeti hivyo walivyotengenezewa kwa kuajiriwa serikalini na taasisi
nyingine.
No comments:
Post a Comment