
Akizungumza
na Wikienda, Jokate alifunguka kuwa anachukizwa na watu wanaotukana wenzao
mitandaoni ndiyo maana uvumilivu ulimshinda na kujikuta akimtolea uvivu mtu
aliyekibeza kidoti chake, akamjibu ndivyo sivyo.
“Unajua
tunawapenda sana mashabiki wetu lakini kuna wakati wanatukosea, unakuta mtu
ametoka alipotoka anakukomentia kitu ambacho siyo, kiukweli sitakubali
kutukanwa, mimi ni mpole lakini sipendi upole wangu unifanye kutukanwa tu,
nitachukua hatua,” alisema Jokate.
Hivi
karibuni Jokate alitupia picha yake mtandaoni ya pozi la uso ambapo mtu mmoja
akamuuliza kama ni kidoti au upele ndipo alipompa jina ambalo lilionekana ni
tusi.
No comments:
Post a Comment