
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala ametangaza operesheni ya usafi na utekelezaji wa sheria ndogo za jiji zilipitishwa tangu mwaka 2014 ili kulifanya jiji hilo kuwa moja ya majiji safi hapa nchini
Hayo
ameyasema leo baada ya kukagua magari 6 ya taka na makontena 91 ya kubebea taka
na kuongea na madiwani, watendaji wa mara na mitaa na kuwataka kusimamia sheria
na vifaa walivyopata kuhakikisha jiji hilo Lina kuwa safi wakati wote

"Magari
tumepata, sheria ndogo ndogo zipo, adhabu kwa watupa taka zipo, adhabu kwa
watiririshaji Maji machafu zipo, nyie viongozi na watendaji mpo sasa
tukasimamie sitaki visingzio na nitapita kila maeneo mahali ambapo pana uchafu
tutaanza na sisi tuliopo hapa nataka jiji safi na la mfano Tanzania"

No comments:
Post a Comment