
Mahusiano
mengi yamekuwa yakivunjika kwa kushindwa kudumu kwa muda mrefu kutokana na kila
mtu kumchoka mwenzake. Unaweza kuwa katika uhusiano kwa muda mrefu na kamwe
usichoke kumwona au kutaka zaidi kutoka kwa mpenzi wako.
Hizi ni njia
tatu zinazoweza kusaidia mahusiano yako kudumu kwa muda mrefu:
Geuza
mtazamo wa mapenzi
Unapaswa
kutumia kila nafasi unayoipata kufanya mapenzi kama nafasi ya kumuonyesha kitu
kipya mpenzi wake – Mwisho utagundua kitu kutoka kwa mpenzi wako huyo!
Jitahidi
kusoma na kujifunza njia mpya kwa ajili ya kumfurahisha mpenzi wako hali
itakayopelekea kumlinda mpenzi wako asitoke nje ya mahusiano yenu.
Watu wengi
wamezoea kuwa mwanaume ndio kiongozi wa kila kitu, hali iliyopelekea mpaka
wanawake wengi hawezi kumuambia mtu wake kuhusu kufanya ‘tendo’ mpaka mwanaume
ndio aanze kusema. Hilo kwenye mapenzi ni kitu ambacho kinapaswa kuwekwa kando
ili kuleta furaha kwenye mapenzi yenu.
Tafuta
ushauri
Kuna mbinu
nyingi ambazo wapenzi hudhani wanazijua, lakini ni njia moja ya kuhakikisha
kuwa mapenzi yananoga kila siku ni kutafuta mbinu mpya na za kipekee.
Wapenzi
wengi wamekuwa waoga kuomba ushauri kama kuna matatizo ndani ya mahusiano yao,
hali inayopelekea mtu huvumilia matatizo hayo mpaka mwisho wake huamua
kulisaliti penzi lake kwa kutafuta furaha kwa mtu mwingine.
Kwenye
mapenzi siyo kila rafiki wala mtu wako wa karibu anaweza kukupa ushauri mzuri
utakaokufaa – Kuna wengine watakushauri vibaya ukajutia maamuzi yako hapo
mbeleni. Unaweza kuwafuata watu waliodumu kwenye mahusiano kwa muda mrefu
wakiwa na furaha na kuweza kuomba ushauri kujua wamefanyaje mpaka kufikia hapo
ili uweze kufikia malengo na mpenzi wako.
Jua vitu
anavyovipenda/ havipendi mpenzi wako
Unapaswa
kuvijua vitu ambavyo havipendi mpenzi wako ili kujiepusha na kumkwaza mara kwa
mara ili hata ikitokea hivyo ujue kwa wakati huo yupo kwenye ‘mood’ gani.
Aidha
wapenzi wengi wamekuwa hawa fahamu sehemu za wapenzi wao zinazowasisimua na
kupandisha raha au kumfikisha ‘kileleni’. Hali hiyo imepelekea wapenzi wengi
kushindwa kudumu kwa muda mrefu kwenye mahusiano yao.
No comments:
Post a Comment