
MREMBO
aliyeingia kwa mbwembwe nyingi kwenye game la muziki Bongo, Helen George
‘Ruby’, hatimaye uongozi wa Tanzania House of Talent ‘THT’, umeshindwa
kuendelea kuvumilia maovu yake na kulazimika kumtimua.
Chanzo cha
kuaminika kilichopo ndani ya taasisi hiyo kilitutonya kuwa, kutimuliwa kwa
binti huyo kumetokana na kukithiri kwa tabia za utovu wa nidhamu jambo ambalo
alikuwa akionywa mara kwa mara na uongozi bila kubadilika.
“Ruby katimuliwa
THT, chanzo ni utovu wa nidhamu anaouonesha. Hana shukurani, imefika wakati
akifanyiwa ‘intaviu’ anakuwa mgumu kuonesha kuwa anatokea THT, anapata shoo
nyingi lakini hana nidhamu ya pesa, kwa hiyo uongozi umeshindwa kumvumilia,”
kilidai chanzo hicho.
Gazeti hili
baada ya kupenyezewa udaku huo lilimtafuta Mkurugenzi Mkuu wa THT, Ruge
Mutahaba ili azungumzie sakata hilo ambapo alijibu kwa kifupi kwamba ni kweli
Ruby amesimamishwa na uongozi baada ya kushindwa kufuata taratibu na sheria za
taasisi hiyo.
No comments:
Post a Comment