KOCHA Jose
Mourinho yupo tayari kuuza hadi wachezaji 13 wa kikosi cha kwanza Manchester
United kwa mujibu wa El Confidencial . Meneja mpya wa United ameripotiwa
kukutana na Mkurugenzi Ed Woodward Ijumaa kujadili mipango yake ya usajili
kuelekea kampeni za 2016/17 na ameorodhesha msururu wa wachezaji ambao hawana
tija.
Juan Mata, Ander Herrera na Memphis Depay wanaongoza katika orodha,
wakati Bastian Schweinsteiger, Marouane Fellaini, Ashley Young, Michael
Carrick,Marcos Rojo na Sergio Romero wapo katika hatari ya kuuzwa. Hata
mustakabali wa Luke katika Old Trafford yupo hatarini kutemwa, ipo wazi kwamba
Mourinho anataka kumtoa kwa mkopo baada ya kukosa karibu msimu mzima kwa
kuvunjika mguu. MustakabaliI Wa Antonio Valencia na Matteo Darmian upo shakani
hali kadhalika. Mchezaji mmoja tu ndo hayupo kwenye hatari ya kuoneshwa mlango
wa kutokea,David De Gea ambaye inafahamika kuwa Mourinho anataka kumbakisha Old
Trafford.
TUPE MAONI YAKO
TUPE MAONI YAKO
ZAIDI TEMBELEA>>> BLOG SPORT
No comments:
Post a Comment