
Watu watatu
wanaosadikiwa kuwa majambazi,wameuawa katika majibizano ya risasi na askari
polisi mkoani Mwanza,alfajiri ya kuamkia jana jumapili katika mapango ya mlima
wa Utemini yaliyopo kata ya Mkolani jijini Mwanza.
Kamanda wa
polisi mkoani Mwanza Ahmed Msangi,amewataja majambazi waliouwa katika
majibizano ya risasi usiku kucha kuwa ni Omar Francis Kitaleti mkazi wa Nyegezi
Kona,said Khamis Mbuli maarufu kama fundi bomba mkazi wa bugarika na jambazi
mwingine ambaye jina lake bado halijafahamika.
Amesema
majambazi hayo yalikuwa yamejificha kwenye mapango ya mlima wa Utemini kabla ya
askari polisi kufanikiwa kuyaua.
Jambazi
mmoja aliyeuawa ambaye hajafahamika jina lake mwenye umri kati ya miaka 20 hadi
25 alikuwa akiwashambulia polisi kwa kutumia bastola ambapo baada ya polisi
kumpiga risasi walimpekua na kumkuta akiwa na bastola aina ya Chinese,iliyokuwa
na risasi tatu ndani ya magazine,huku majambazi wengine waliokuwepo kwenye
mapango hayo wakiendelea kujibishana kwa risasi na askari polisi.
Kamanda
Msangi ameongeza kwamba Ijumaa Juni 3,askari polisi kwa kushirikiana na vyombo
vya ulinzi na usalama,walimkamata Omar Francis Kitaleti kwa jina maarufu
kiberiti,mkazi wa Nyegezi Kijiweni ambaye alikuwa akituhumiwa kuhusika katika
matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha kwenye maduka ya M-pesa,Tigo Pesa na
Airtel money jijini Mwanza ambaye baada ya kuhojiwa alikiri kuhusika katika
matukio hayo na aliwataja wenzake anaoshirikiana nao na mahali walipojificha.
hayo.

Omary
Francis Kitaleti @Kiberiti, mmoja wa majambazi aliyeuawa na wenzake kwa risasi.
Katika
mapambano hayo ya risasi na askari polisi,risasi hizo ziliweza kumpata jambazi
mwenzao aitwaye Omary Francis Kitaleti aliyekuwa anawaongoza askari polisi na
kufariki dunia papo hapo, na risasi nyingine ilimjeruhi askari kwenye unyayo wa
mguu wake wa kulia.
Amesema
polisi kwa kutumia mbinu za medani za kivita waliweza kuzingira maeneo hayo ya mlima
wa utemini hadi alfajiri ya kuamkia Jumapili Juni 5,huku wakijibishana risasi
na majambazi hao na baada ya kuona yamezidiwa nguvu huku kukikaribia
kupambazuka ndipo yalipoamua kuondoka ndani ya mapango hayo kwa kurusha bomu
moja la kutupa kwa mkono huku yakizidisha mapigo ya risasi kwa kutumia silaha
walizokuwa nazo.
Ameongeza
kuwa polisi wamekamata bunduki moja aina ya SMG iliyokuwa na risasi nane na
kisu kimoja.
Kamanda
Msangi amesema majambazi watatu walifanikiwa kutoroka kutoka kwenye mapango
hayo kuelekea maeneo ya Nyasaka na baada ya jambazi mmoja kubaini kuwa askari
polisi walikua wanamfuatilia alitoa bunduki
na kutaka kuwapiga askari polisi lakini polisi waliweza kumuwahi na
kumfyatulia risasi sehemu mbalimbali za mwili wake na kufariki dunia papo hapo.
Amesema
askari polisi wamefanya upekuzi kwenye mapango ya mlima wa Utemini na
kufanikiwa kupata vitu mbalimbali vilivyoachwa na majambazi hao ambavyo ni pamoja
na risasi nne,kisu kimoja chenye damu,kofia ya kuficha uso nyeusi moja
(mask),jiko la stove,masufuria ya kupikia, unga wa mahindi,sukari,dagaa,chakula
kilichopikwa,ngoma mbalimbali,na simu tatu za mkononi.
Askari
aliyejeruhiwa amelazwa hospitali ya rufaa ya bugando na hali yake inaendelea
vizuri,polisi bado wanaendelea na msako wa kuwatafuta majambazi waliofanikiwa
kutoroka.
Mkuu wa mkoa
wa Mwanza John Mongella, akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo
alitembelea kwenye mapango ya Utemini na kuwaomba wananchi kuendelea kutoa
ushirikiano kwa jeshi la polisi katika kuwafichua wahalifu
No comments:
Post a Comment