Takriban
watu 17 wanahofiwa kufariki baada ya moto mkubwa kutokea katika jumba moja la
makaazi ya kuwahudumia wakongwe, karibu na mji mkuu wa Ukraine, Kiev.
Wakuu
wanasema kuwa idara ya huduma za kuwaokoa watu ilifaulu kuwaokoa watu wengine
17, watano kati yao wamekimbizwa Hospitalini, wakiwa na majeraha mabaya ya
moto.
Taarifa
kutoka huduma ya zima moto mjini humo, zinasema kuwa moto huo ulitokea mapema
leo Jumapili, katika jumba moja la kibinafsi lililoko karibu na makao hayo,
ambayo yalikuwa yakiwahudumia kwa muda watu 35, kutoka katika kijiji kimoja
kilichoko hapo karibu.
No comments:
Post a Comment