
Msanii wa
filamu nchini ambaye anafahamika kwa kuigiza kwa lafudhi ya Kimakonde Gambo
Zigamba amefunguka na kusema kuwa yeye ni zaidi ya msanii Ray Kigosi kwenye
kazi kwani yeye anafanya zaidi ya Ray.
Akizungumza
kwenye kipindi cha eNewz Gambo Zigamba aliweka wazi kuwa kipindi ambacho wakina
Ray na wasanii wengine wakongwe wanafanya kazi zao hizo kulikuwa hakuna wasanii
wengine wachanga ndiyo maana walikuwa wanaonekani ni wazuri sana lakini hivi
sasa tasnia imekuwa na vipaji vipya ambavyo vinafanya vizuri zaidi yao hao wakongwe.
Mbali na
hilo msanii huyo alikubali kuwa msanii Ray Kigosi ana ladha zake katika kazi na
ana mashabiki wake katika tasnia hiyo ila anachoamini yeye ni zaidi ya Ray
Kigosi na kusema wapo watu wana uwezo wa kufanya kitu zaidi ya huyo Ray.
"Ray
ana flavor (ladha) zake na wapo watu wapo wanampenda Ray lakini kuna watu zaidi
ya Ray wanaweza kufanya vizuri zaidi ya Ray, ila naweza kusema mimi ni zaidi ya
Ray kwani naweza kufanya kitu zaidi ya Ray, Ray akabaki amefanya na mimi
nikafanya zaidi yake na watu wakapenda zaidi. Mimi siogopi mtu japo ukweli
utabaki pale pale kuwa baba ni baba ila mtoto anaweza kufanya jambo vizuri hata
zaidi ya baba yake," alijigamba Zigamba.
No comments:
Post a Comment