Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR)
limeitaja nchi ya Sudan Kusini kuwa nchi ya tatu duniani kwa kuwa na idadi
kubwa ya wakimbizi.
Sudan Kusini imeshika nafasi hiyo, ikiwa nyuma ya Syria na
Afghanistan ikiwa na wakimbizi wanaokadiriwa kufikia milioni 1.5 na zaidi ya
wananchi milioni 2.1 wa nchi hiyo wakiwa wamekimbia makazi yao.
UNHCR imesema kuwa kwa mwaka 2017 pekee, shirika hilo la wakimbizi linahitaji
Dola milioni 782 (Trilioni 1.7 ya Kitanzania) kwa ajili ya kuhudumia wakimbizi
pekee wa Sudan Kusini.
Msemaji wa UNHCR, William Spindler alisema kwa nusu ya
kwanza ya mwaka 2016 kulikuwa na wakimbizi 760,000 wa Sudan Kusini na nusu ya
pili waliongezeka 500,000.
Aidha Spindler alisema asilimia 60 ya wakimbizi hao ni
watoto na kwa mwaka 2017 wanategemea idadi ya wakimbizi kuongezeka kwani bado
hakuna juhudi za uhakika zinazofanyika kurudisha hali ya usalama wa uhakika
kuwa kama jinsi ilivyokuwa awali.
Kwasasa Sudan Kusini ina wanajeshi 13,500 wa Umoja wa
Mataifa (UN) ambao wanalinda amani na UN mwezi Januari ilitaka kuongeza
wanajeshi 4,000 lakini serikali ilikataa.
No comments:
Post a Comment