
Serikali imesema itanunua rada nne ambazo zitawekwa sehemu
mbali mbali za Tanzania ili kuwezesha kuona aina yoyote ya ndege inayoingia ama
kupita katika anga la Tanzania ili kuhakikisha nchi ya Tanzania inakuwa salama
mda wote.
Akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mtwara waziri wa ujenzi
uchukuzi na mawasiliano Professor Makae Mbalawa ambae ametembelea uwanja wa
Ndege,kivuko cha mpakani mwa Tanzania na msumbiji cha Mvi Kilambo pamoja na
bandari,amesema kuwa kwa sasa serikali imefikia uamuzi huo wa kununua rada nne
kwa kuwa kuna maeneo mengine hayaonekani katika rada iliyopo.
Aidha rada hizo zitasaidia kuona ndege ndogo ndogo ambazo
zinatua katika migodi ya madini ambazo hazijulikani zinabeba nini.
No comments:
Post a Comment