Mwanamke mwenye umri wa miaka 64 amefanikiwa kujifungua
mapacha -mvulana na msichana katika eneo la Burgos, kaskazini mwa Uhispania.
Hospitali ya Recoletas iliwapokea watoto hao kupitia
upasuaji ,ambapo hufanyika husuasan wakati wa visa kama hivyo.
Mwanamke huyo ambaye hakutajwa amefanyiwa matibabu ya uzazi
nchini Marekani kulingana na vyombo vya habari vya Uhispania.
Hospitali hiyo imechapisha kanda ya video kuhusu upasuaji
huo. Mwaka 2012 mwanamke huyo alijifungua mtoto wa kike ambaye baadaye
alichukuliwa na kulewa na huduma za kijamii licha ya wasiwasi kuhusu hali yake.
Wafanyikazi wa kijamii wanasema kuwa msichana huyo alilewa
akiwa pekee ,akiwa na mavazi mabaya mbali na uchafu wa eneo alilokuwa.
Hakuna uamuzi uliochukuliwa kufikia sasa kuhusu mama ya
mtoto huyo.
Yeye na mamake wanadaiwa kuwa katika afya nzuri hospitalini.
Mvulana huyo ana uzito wa kilo 2.4 huku msichana akiwa na uzito wa kilo 2.2.
Mama huyo alijifungua bila matatizo yoyote. Katika siku za
hivi karibuni, wanawake wengine wawili wa Uhispania wamejifungua watoto wenye
afya.
Mnamo mwezi Aprili 2016 mwanamke mmoja wa Kiindi aliye na
umri wa miaka 70 Dajlinder Kaur ,alijifungua mtoto mwenye afya katika jimbo la
Haryana nchini India baada ya kufanyiwa ukaguzi wa kizazi chake.
No comments:
Post a Comment