
KIONGOZI wa madansa ambaye ni dansa tegemezi wa Wasafi
Classic Baby (WCB) Mose Iyobo amefunguka kuwa yeye hana imani na Harmorapa na
anashangaa anavyotajwa kila mahali kwani yeye hajawahi kusikia kazi yake yoyote
hivyo hajui uwezo wake kimuziki.
Iyobo aliendelea kwa kutoa povu kuwa yeye anamchukulia
Harmorapa kama mtu aliyekurupuka kwenye muziki na hajui ni nini anachotakiwa
kufanya.
Kupitia eNewz ya EATV Iyobo alifunguka hayo huku akikazia
kuwa muziki si jambo la mchezo mchezo bali unahitaji kujipanga.
“Mimi ni mtu ambaye nipo kwenye muziki muda mrefu, kila siku
nyimbo mpya zinapotoka ziwe za watu maarufu hata wasio maarufu nazisikia lakini
mimi sijawahi kusikia kazi yoyote ya Harmorapa, kwa hiyo sina cha kumshauri ila
hiyo kazi anayofanya inahitaji mtu makini, anayekwenda na wakati na siyo
kukurupuka tu na kufanya ghafla sababu hiyo kazi ina pesa nyingi na inatia
umasikini kwa haraka sana kama hufanyi vile inavyotakiwa,” alisema Mose Iyobo
No comments:
Post a Comment