Wakati klabu ya Liverpool ikiwa katika fomu mbovu kutokana
na kutokupata ushindi katika mwezi januari kwenye ligi kuu ya Uingereza,
Taarifa zinasema klabu hiyo ilikuwa inunuliwe na tajiri namba moja duniani na
mmiliki wa Microsoft Bill Gates pamoja na mmiliki wa mabingwa wa kihistoria wa
Super Bowl, New England Patriots bwana Robert Kraft kipindi ambacho waliokuwa
wamiliki wa klabu hiyo Tom Hicks na George Gillett walipoamua kuiuza.
Taarifa zimetolewa na nyaraka zilizopatikana katika mahakama
kutokana na taarifa za ushindani wa kisheria kati ya kampuni inayofahamika kama
Mill Financial and Gillett na ile ya Royal Bank of Scotland. Hicks na Gillett
walikubali kuiuza Liverpool mwezi April 2010 baada ya kushindwa marejesho ya
fedha walizokopa wakati wanainunua klabu hiyo mwaka 2007.
Barclays Capital walipewa kazi ya kutafuta wanunuzi, na
nyaraka kutoka kwenye kanda ya kiuchumi katika mahakama kuu ya New York County
Supreme Court zinaonyesha kuwa Bill Gates, mwanzilishi wa Microsoft, alifuatwa
katika yangazo la wahitaji wa kuinunua klabu hiyo.
Martin Broughton, ambaye alikuwa mwenyekiti wa Liverpool
kipindi hicho, aliulizwa kama kulikuwa na ukweli juu ya kufuatwa kwa Bill Gates
na Bob Kraft, akajibu “ni kweli kabisa”
Broughton aliulizwa pia kama alikuwa anafahamu kama Barclays
Capital walikuwa wanafuatilia jitihada zilizokuwa zinafanywa na wawekezaji wa
Hong Kong, Norway.
Alijibu kwa kusema, utafutaji wa wawekezaji wapya ulifanyika
katika kila bara na ulihusu kuwasiliana na watu tofauti duniani kote. Bill Gates hakujibu au kuitikia wito lakini
Kraft alisita katika kuinunua klabu hiyo huku pia akiwa alikataa ofa ya David
Moores mwaka 2005.
New England Sports Ventures, wanaofahamika kama Fenway
Sports Group, hatimae waliinunua Liverpool kwa dau la £300 million mwezi
October 2010, huku Hicks na Gillett wakisema dili lile lilikuwa wizi wa mchana.
No comments:
Post a Comment