Msanii wa muziki wa hip hop kutoka Morogoro Afande Sele
amesema leo tafsiri ya msemo wake ‘wasafi wataonekana wachafu’ ambayo aliitoa
siku za karibuni baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kutangaza
awamu ya kwanza ya majina ya watu ambao wanatuhumiwa kujihusisha na matumizi ya
Madawa ya kulevya.
Kauli hiyo ilitafsiriwa vibaya na mashabiki wa Diamond wengi
wakidhani mkongwe huyo naye naamini kwamba WCB wapo kwenye sakata hilo.
Kupitia list mpya ya RC Makonda ambayo ameitoa leo na kutaja
majina ya watu wakubwa akiwemo Yusuph Manji, Mchugaji Ngwajima, Iddi Azzan na
wengine, Afande Sele ameweka bayana nini alikuwa anakimaanisha kwenye kauli
yake hiyo.
“Juzi kati niliposema kuwa kwenye hili sakata la MAPAPA na MAPUNDA wa’Unga’kama kweli braza Paul yupo’serious’….basi hata wale WASAFI wataonekana WACHAFU….wenye akili zao timamu walinielewa vyema….lkn vibichwa panzi walitafsiri kiudaku na kichonganishi tu wakimaanisha neno wasafi na wale wasafi wao wa mbagala…nadhani sasa tumeanza kuelewana…..NAONA MBALI KWA DARUBINI KALI…..wacha ‘parry’iendelee,” aliandika rapper huyo Instagram.
No comments:
Post a Comment