Maandamano ya wanawake dhidi ya Donald Trump, yamefanywa
nchini Australia, New Zealand na Japani.
Maandamano makubwa kabisa hadi sasa yamefanywa Sydney,
Australia, ambako watu kama elfu tatu wanaopinga ile inayosemekana kuwa tabia
ya Bwana Trump, ya kunyanyasa wanawake, waliandamana hadi ubalozi mdogo wa
Marekani mjini humo.
Waandamanaji walisema wanataka kumulika haki za wanawake na
wachache, ambazo wanasema, zinakabiliwa tishio.
Maandamano zaidi yanayoitwa maandamano ya madada yanapangwa
kufanywa sehemu mbali mbali za dunia.
Mkusanyiko mkubwa unatarajiwa mjini Washington, ambako
ma-elfu wanatarajiwa kufanya mhadhara.
Baada ya Bwana Trump kuapishwa, maandamano yamefanywa
kwengineko na Marekani, pamoja na huko Seattle, ambako mtu mmoja alipigwa
risasi na kujeruhiwa.
Mjini Nairobi kundi moja la waandamanaji wakiwemo Wamarekani
na raia wa Kenya walikongamana kushiriki katika matembezi ya wanawake ili kupinga
unyanyansaji wa kingono na ukosefu wa usawa wa kijinsia mbali na kutaka
kushirikishwa katika maswala zaidi ya maendeleo na uongozi.
No comments:
Post a Comment