Mbwa ambaye alimeza kisu cha urefu wa sentimita 20 anapata
nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji.
Mbwa huyo wa umri wa wiki 12 kwa jina Macie, alikimbizwa kwa
daktari wa mifugo kwa huduma ya dharura baada ya kuanza kukohoa.
Mwenye mbwa huyo anasema alidhani kuwa alikuwa amemeza kifaa
cha kuchezea cha watoto, lakini X ray baadaye ilionyesha picha ya kisu kikuwa
tumboni.
Daktari ambaye amekuwa akimtunza mbwa huyo tangu afanyiwe
upasuaji anasema ana habati sana kuwa hai.
Mwenye mbwa huyo kutoka Glasgow alikuwa amempoteza mbwa wake
mwingine kutokana na ugonjwa wa saratani
Siku moja baada ya kufanyiwa upusuaji alionekana mchangamfu.
Mbwa huyo amekuwa akirudishwa kwa daktari kufanyiwa ukaguzi kwa muda wa wiki
mbili na sasa anaendelea kupata nafuu.
No comments:
Post a Comment