
Shirikisho la Kandanda nchini Tanzania TFF limesema kuwa
limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha David Burhan mchezaji wa Kagera
Sugar ambaye mefariki usiku wa kuamkia leo.
Kupitia ukurasa wake wa twitter rais wa shirikisho ls soka
Jamal Malizi aliandika haya "Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha
David Abdalah Burhan mchezaji wa Kagera Sugar.Amefariki usiku wa kuamkia
leo.Apumzike kwa amani.alisema Malizi.
Mapema hibvi leo taarifa za msiba wa Kipa wa Kagera Sugar,
David Burhani zilianza kuvuma haswa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii
kwamba amefariki dunia.
David Buruhan kipa wa Kagera Sugar na mtoto wa Mshambuliaji
wa zamani wa PAN Abdallah Buruhan amefariki katika Hospital ya Bugando jijini
Mwanza alikokuwa amelazwa baada ya kusumbuliwa na Malaria, Burhani aliwahi
kuichezea Mbeya City na baadaye aliweza kujiunga na Majimaji ya Songea na
kuitumikia msimu mmoja.
aarifa zaidi endelea kufuatilia taarifa zetu.


No comments:
Post a Comment