
Wabunge na mawaziri wametii agizo la Spika wa Bunge, Job
Ndugai lililowataka kuzingatia mahudhurio ya vikao vya kamati za Bunge,
vinginevyo majina yao yangewasilishwa kwa mamlaka wanazowajibika ikiwamo kwa
Rais John Magufuli.
Katika mkutano wa nne wa Bunge mwaka jana, Spika Ndugai
alisikitishwa na mahudhurio hafifu ya mawaziri na wabunge katika vikao vya
kamati vilivyofanyika kuanzia Septemba 22 hadi Oktoba 2 mjini Dodoma.
Amesema katika vikao hivyo vya kamati ilitengenezwa orodha
ya wabunge na mawaziri watoro, ambayo
ataitunza hadi vikao vingine vya kamati.
Spika Ndugai aliwaonya kuwa
iwapo wataendelea na tabia ya utoro kwa vikao vya kamati vilivyofanyika
kati ya Oktoba 17, 2016 angewashtaki kwa
wapigakura, vyama vyao na mawaziri angewafikisha kwa Rais Magufuli.
No comments:
Post a Comment