
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA),
John Brennan amemuonya Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump kuwa makini na
kauli zake na kuuchunga mdomo wake, hasa anapozungumzia suala la uhusiano wa
kidiplomasia kati ya Marekani na Urusi kwa madai kwamba anahatarisha usalama wa
Taifa la Marekani.
Brennan aliendelea kueleza kuwa, Trump bado hajaelewa nia ya
Urusi kwa Marekani kwa hiyo badala ya kufurahia mipango ya siri inayoendelea,
anapaswa kuwa makini na kuchunga kauli zake.
“Nafikiri Trump haelewi kwa sababu gani uhusiano wa Marekani
na Urusi umekuwa suala tete kwa kipindi kirefu kilichopita, anatakiwa kuwa
makini sana anapolishughulikia suala hili,” alisema na kuongeza kuwa CIA inazo
taarifa za namna Urusi inavyojaribu kumtumia Trump kutimiza matakwa yake.

John Brennan
Brennan aliyazungumza hayo wakati akihojiwa na Kituo cha
Runinga cha Fox News, ikiwa ni wiki moja tangu alipotangaza ripoti kwamba
wamegundua kuwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin na vijana wake, walifanya
‘makeke’ ili Trump ashinde kwenye uchaguzi mkuu nchini humo, na kumuangusha kwa
hila mpinzani wake, Hillary Clinton.
No comments:
Post a Comment