October 31 2016 Tanzania ilimpoteza bondia maarufu wa ngumi
za kulipwa Thomas Mashali ambapo
ilielezwa kuwa Marehemu Mashali alifariki usiku wa kuamkia October 31 2016
maeneo ya Kimara Dar es salaam kwa kushambuliwa na watu baada ya kusingiziwa ni
mwizi na watu ambao aligombana nao.
Leo December 8 2016 kwa mara ya kwanza watuhumiwa wa mauaji
ya bondia huyo wamefikishwa mahakama ya
hakimu mkazi Kinondoni na kusomewa shitaka hilo la mauaji, kesi hiyo itatajwa
tena December 20 2016 na watuhumiwa wote wamerudishwa rumande.
No comments:
Post a Comment