CHIKI 'Ampigia Magoti' JB Baada ya Kusikia Ameacha Kuigiza Bongo Movies - boazmwakasege.com

MADA MOTO

Monday, December 5, 2016

CHIKI 'Ampigia Magoti' JB Baada ya Kusikia Ameacha Kuigiza Bongo Movies

 
Msanii wa bongo movie Chiki amesema JB hana sababu ya kustaafu kuigiza kwa kuwa ni mtu ambaye bado sanaa inamuhitaji na kuna wasanii wachanga na wakongwe wanamuhitaji kwa ushauri zaidi.

Akiongea kupitia eNewz Chiki amesema anamkumbusha JB kurudi bongo movie kwa kuwa sanaa haina kustaafu na kama kuna malengo ambayo aliyaweka yakawa hayajatimia asikate tamaa arudi kuendeleza chipukizi ambao wanakuwa lakini pia kama malengo yake yametimia basi awasaidie na waliopo chini yake.

SOMA HAPA ====>>>>>>>   BONGO Movie Yazidi Kufa, JB Nae Aacha Kuigiza


Pia Chiki amesema hana mpango wa kustaafu kuigiza kwa kuwa anaamini kuwa kuna mashabiki zake ambao bado wanatamani kuona kazi zake na wanamkubali lakini pia anajipanga ili kuirudisha bongo movie kama zamani.

No comments:

Post a Comment