Ni baada ya show ya Fiesta Dar es Salaam ndipo Nikki wa Pili
alisikika akimmwagia sifa kibao Abdul Kachaa almaarufu kama Dogo Janja na kudai
kuwa ndiye msanii wake bora wa mwaka.
Yalisikika mengi kwa upande wa Weusi pamoja na Dogo Janja
ikiwemo issue ya kufanya kazi pamoja na vitu kama hivyo lakini Madee Ali ambaye
ndiye mlezi wa Dogo Janja alikuwa hajasikika kokote kuhusiana na suala hilo.
imemtafuta raisi wa
manzese Madee na kupiga nae story kuwa analizungumzia vipi suala hilo la Dogo
Janja kufanya kazi na Weusi, na Madee alikuwa na haya ya kusema.
“Hiyo ni biashara ambayo iko kwenye engo ningine kabisa,
kama Dogo Janja ataamua yeye kama yeye mimi wala sitokuwa na shida kwasababu
anaweza kuwa anaona kule kuna kitu ambacho atakuwa anakipata tofauti na huku
ambako ameishi, me nadhani ntampa uhuru tu na kumtakia mafanikio mema. Lakini
kama ni biashara nyingine ambayo hao anaotaka kufanya nao biashara watataka
kufanya na Dogo Janja basi itabidi waufuate uongozi wa Tiptop Connection.”
No comments:
Post a Comment