Sanamu mbili
mpya za kiongozi wa muda mrefu wa Zimbabwe Robert Mugabe zimezinduliwa mjini
Harare.
Sanamu hizo,
ambazo zilizinduliwa katika ikulu ya rais zimetayarishwa na mchongaji sanamu
maarufu Dominic Benhura.
Rais Mugabe
ameeleza kufurahishwa na sanamu hizo mbili kwa mujibu wa gazeti la serikali The
Herald.
"Hii ni
kazi nzuri Sanaa ya Sanaa na wasanii walioshiriki inaonekana wana vipaji adimu,
wana vipaji kwa kweli," amenukuliwa Bw Mugabe.
Bw Benhura
ameoneshwa kwenye picha zilizochapishwa na gazeti la The Herald akiwa amesimama
karibu na sanamu hiyo akiwa na Bw Mugabe na mke wa rais Dkt Grace Mugabe.
Sanamu hiyo,
ambayo urefu wake ni karibu maradufu kimo cha Rais Mugabe, inamuonesha kiongozi
huyo wa umri wa miaka 92 akiwa na miwani yake maarufu, masharubu na akiwa
ameinua mkono akiwa ameufumbata kama ngumi.
Baadhi ya
raia nchini Zimbabwe hata hivyo hawajapendezwa na sanamu hizo na wanasema
zinaonekana kama vibonzo.
"Robert
Mugabe ametukanwa kwa sanamu hii na bado hajaelewa," mmiliki wa gazeti
ambaye pia ni mwanaharakati Trevor Ncube ameandika kwenye Twitter.
"Ningelikuwa
Robert Mugabe yule mtawala wa kiimla, ningeamuru (Benhura) akamatwe na niue
sanamu
Bw Mugabe
amesema anataka kuongoza Zimbabwe hadi kifo kimchukue.
Wengine hata
hivyo wamemtetea, akiwemo waziri wa sayansi Jonathan Moyo ambaye ameandika
kwenye Twitter: "Wachongaji vinyago Zimbabwe wana uhuru wa kisanaa. Mvuto
wa sanaa umo kwenye anayetazama. Benhura ni mchongaji vinyago
anayeheshimika!"
Msanii huyo,
ambaye anasema ilimchukua miezi sita kutengeneza sanamu hizo za Bw Mugabe, pia
amejitetea.
"Nilipokea
wajibu huu na nikafanya kadiri ya uwezo wangu. Kawaida, kazi yangu si
kutengeneza picha (kazi za Sanaa) za kuashiria sura za watu. Bila shaka,
hazikutokea kama wengi walivyotarajia," Benhura ameambia shirika la habari
la AFP.
Bw Mugabe
ameongoza Zimbabwe tangu 1980.
chanzo: BONGOSWAGGZ
No comments:
Post a Comment