September 3
2016 ni siku ambayo timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ilicheza mchezo wake
wa mwisho wa kuwania kucheza michuano ya mataifa ya Afrika 2017 na timu taifa
ya Nigeria katika uwanja wa Uyo uliyopo katika jimbo la Akwa Ibom State.
Katika
mchezo huo ambao ulikuwa wa kukamilisha ratiba kwa timu zote mbili Taifa Stars
walifungwa goli 1-0 goli ambalo lilifungwa na nyota wa Man City Kelechi
Iheanacho dakika ya 77 ya mchezo baada ya kupiga shuti lililomshinda golikipa
wa Tanzania Aishi Manula, licha ya kufungwa Taifa Stars walionesha uwezo mkubwa
wa kupambana kiasi cha gavana wa jimbo hilo kuwapa zawadi.
Gavana wa
jimbo la Akwa Ibom State alitoa zawadi ya dola 10000 ambazo ni zaidi ya Tsh
milioni 21 kwa wachezaji wa Taifa Stars kutokana na uwezo waliouonesha, fedha
hizo walipewa katika hafla ya chakula cha pamoja baada ya mchezo huo.
CHANZO:
Shaffihdauda
No comments:
Post a Comment