Jackie Chan kukabidhiwa tuzo ya heshima ya Oscar Novemba mwaka huu - boazmwakasege.com

MADA MOTO

Friday, September 2, 2016

Jackie Chan kukabidhiwa tuzo ya heshima ya Oscar Novemba mwaka huu

Jackie Chan 2
Wengine wanaotarajiwa kupewa tuzo kama hiyo kwa mchango wao kwenye filamu ni pamoja na mhariri wa filamu za Uingereza, Anne V. Coates, muongozaji wa filamu Lynn Stalmaster na muandishi wa makala Frederick Wiseman.
Rais wa jopo lililohusika kuwateuwa watu hao, Cheryl Boone Isaacs amewataja watu hao kama ni waasisi halisi kwenye tasnia hiyo ya filamu.
“True pioneers and legends in their crafts,” amesema Cheryl. Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika mwezi Novemba, mwaka huu huko Los Angeles.
Mwaka 2016 umekuwa wa neema kwa muigizaji huyo kutokana na hivi karibuni kuorodheshwa kwenye jarida la Forbes kama muigizaji anayeshika namba mbili kwa kulipwa zaidi kwenye filamu akiwa anaingiza kiasi cha $61m

KAMA BADO HUJASOMA KURASA ZA MAGAZETI YA LEO, NIMEKUSOGEZEA MTU WANGU
BONYEZA HAPA CHINI:

No comments:

Post a Comment