MAKAMU wa
Rais, Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Awamu ya Tano, itapambana kwa
nguvu zote na vitendo vya ufisadi kwenye fedha, zinazoelekezwa kwenye miradi ya
maendeleo.
Amesema
serikali ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za
kijamii kwa kuendelea kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi, kudhibiti
matumizi yasiyo lazima na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa kodi ili fedha
zinazokusanywa, zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi.
Alisema hayo
jana wakati akifunga maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima ya Nanenane kitaifa
katika Uwanja wa Ngongo mkoani Lindi kwa niaba ya Rais John Magufuli.
Katika
hotuba yake kwa mamia ya wananchi waliofurika katika viwanja hivyo, Makamu wa
Rais alisema azma ya serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo itatimia, iwapo
tu vitendo vya ufisadi katika fedha zinazoelekezwa kwenye maendeleo utakoma.
Alisema pia
hayo yatawezekana endapo wananchi wataunga mkono jitihada za serikali katika
kulipa kodi kwa wakati, kudai risiti, kufanya kazi kwa bidii na kukemea vitendo
vya rushwa kama hatua ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2020.
No comments:
Post a Comment