Rais
Magufuli alisema pamoja na Watanzania wote kuungana kuombea amani na utulivu,
pia hawana budi kutekeleza kwa vitendo maandiko matakatifu ya Biblia yasemayo
“Asiyefanya kazi na asile” kwa kuhakikisha kila mmoja anachapa kazi kwa juhudi
na maarifa ili kuharakisha maendeleo ya Taifa.
“Ndugu zangu
nawashukuru sana, muendelee kuliombea taifa hili, taifa letu ni la umoja, sisi
wote ni Watanzania, tuendelee kumuomba Mola wetu, kudumisha amani yetu, kujenga
umoja wetu kwa dini zote, makabila yote na vyama vyote, kwa sababu Mola wetu
anatupenda sisi sote,” alisema Rais Magufuli.
Aidha, baada
ya kuwasalimu waumini wa Kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato, Rais
Magufuli aliendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo jipya la kanisa hilo,
ambapo Sh milioni moja zilikusanywa papo kwa hapo.
RAIS John
Magufuli ametembelea msikiti na makanisa yaliyopo Chato mjini mkoani Geita na
kuendelea kuwasihi Watanzania kuombea amani na utulivu katika nchi, bila kujali
tofauti za dini, makabila na kanda wanazotoka.
Rais alitoa
ujumbe huo mara baada ya kusali ibada ya Jumapili katika Kanisa Katoliki la
Bikira Maria Parokia ya Chato. Baadaye alitembelea Kanisa la Anglikana la
Mtakatifu Stephano Parokia ya Chato, Kanisa la African Inland Church la Chato
na kumalizia katika Msikiti wa Omar Bin-L-Khattab wa Chato.
No comments:
Post a Comment