Kumewahi
kuwa na tetesi miaka ya nyuma kuwa msanii wa rap toka Kenya, Prezzo alikuwa
anatoka kimapenzi na mtangazaji maarufu wa clouds FM,Diva kutokana na ukaribu
waliokuwa nao mpaka kufikia hatua ya mtangazaji huyo kujichora tattoo ya
Prezzo.
Alipoulizwa
kuhusiana na tetesi hizo kwenye kipindi cha Funiko Base cha radio 5,Prezzo
alidai kuwa yeye na Diva zaidi ya kuwa washikaji hawajawai kujihusisha kwenye
mambo ya mapenzi kama watu wengi wanavyodai.
“Mimi na
Diva hatukuwahi ku date,tulikuwa washikaji.Sema bloggers wanaongeza chumvi kwa
sababu tulikuwa close friends ila hatujawai ku date hata denda sijawahi kula
bado” alifunguka Prezzo.
Alipoulizwa
suala la mtangazaji huyo kujichora tattoo yake Prezzo alisema,”Alijichora
tattoo si kwa vile mimi ni mshkaji wake,haimaanishi kulikuwa na kitu zaidi ya
urafiki,kama ningekula vitu ningekula vitu ningesema tu sasa hivi“.
Moja ya
picha iliyowahi kusambaa na kuchochea tetesi za wawili hao kuwa na mahusiano ya
kimapenzi
No comments:
Post a Comment