LILE andiko
la usimjaribu bwana Mungu wako lililosemwa na Yesu Kristu limejidhihirisha
baada ya mchungaji maarufu nchini Afrika Kusini, Alfred Ndlovu (44), kufariki
dunia baada ya kufunga usiku na mchana kwa takribani siku 30 akitaka kuvunja
rekodi ya Yesu Kristu aliyefunga siku 40 bila kula kitu chochote.
Kama
alivyofanya Yesu Kristu, Mchungaji Ndlovu naye aliondoka nyumbani kwake
Juni 17 mwaka huu na kuelekea nyikani
kwa ajili ya kufunga na kuomba, huku akiweka pembeni anasa za dunia.
Kifo cha
mchungaji huyo kimeishangaza sana familia yake, waumini wa kanisa lake na jamii
nzima kwa ujumla.
Mchungaji
huyo alijulikana kwa imani yake thabiti ambayo
ingeweza hata kuhamisha milima.
Mmoja wa
wanafamilia ya mchungaji huyo alisikika akilalamika; “Alikuwa mtu wa imani
sana. Lakini kwa bahati mbaya amefariki kifo hicho. Baada ya mwezi ndipo
tumepata taarifa za kifo chake”
Akijaribu
kuvunja rekodi ya Yesu, Mchungaji Ndlovu alifariki baada ya kufunga kwa
takribani siku 30 japokuwa hakuwahi kuripotiwa kuwa na ugonjwa wowote hapo
awali. Alikuwa peke yake nyikani na maiti yake iligunduliwa na mpita njia mmoja
aliyetoa taarifa polisi.
No comments:
Post a Comment