Kuna sababu
anuai zinazomfanya mwanamke amsaliti mumewe. Ni muhimu kutambua kuwa mwanamke
ni kiumbe mwenye hisia kali na daima ahisi raha na amani. Baadhi ya nyakati
hufanya usaliti ili kuziba pengo la upungufu unaotokea katika maisha yake.
Zifuatazo ni sababu kubwa ambazo zinamfanya amsaliti mumewe.
Tunatambua
kuwa mke anafanya kazi kubwa sana ambayo kama ingekuwa ni kampuni basi
pangehitajika watu zaidi ya 10 kuzifanya. Atamtunza mume, watoto, nyumba na
familia kwa ujumla.
Wakati fulani mume anaweza akampuuza na
asimthamini, licha ya kujitoa kwa moyo wote kumtunza na kuihudumia familia.
Hivyo, kutotoa kipaumble kwa mke ni kosa kubwa ambalo linaweza likamgharimu
mume, mke akipata mtu anayempa kipaumbele na kumuonesha thamani hakika hataacha
kuitumia hiyo fursa
UKOSEFU WA
MAHABA
Kwa asili
mwanamke anasilika ya hitajio la kupendwa, mwanamke anahitaji kupendwa,
mwanaume yeye ana silika ya kupenda ngono, ukimpa ngono tu basi anaridhika..
Mwanamke
anahitaji kupetiwapetiwa, anahitaji kudekezwa, anahitaji aambiwe maneno yenye
ladha adimu yaliyochanganywa na vionjo vya ndimu, mwanamke anataka hivyo,
anataka aone kama anapendwa, anataka aone mtu anamwambia vile alivyo, alivyo
maridhawa, amueleze hisia zake, ampe lugha ya kimajnun, mwanamke anamtaka
Majnun. Sasa akimpata mtu wa aina hiyo, tofauti na mumewe, huwa ni balaa tupu,
mnanipata hapo?
USALITI WA
MUME
Miongoni mwa
mambo ambayo huibadilisha roho ya mwanamke ni pale anapogundua kuwa mumewe
kipenzi anamsaliti. Hapo mwanamke anaweza akabadilika kabisa. Wapo wanaosamehe,
lakini wapo wanaolipiza kisasi.
KUTOJIAMINI
Mwanamke
anahitaji mwanaume anayemfanya ajiamini iwapo mumewe hatekelezi jukumu hilo,
akimpata mtu anayemfanya ajiamini, yanaweza kutokea mengine kabisa. Hivyo,
nasaha zangu kwa kaka zangu kuyaangalia kwa makini mambo haya.
No comments:
Post a Comment