
Naibu mkuu
wa jeshi la Uturuki ametangaza kwa njia ya runinga kuwa jaribio la mapinduzi ya
kijeshi limeshindwa.
Jenerali
Umit Dundar alisema kuwa wapanga mapinduzi 104 wameuauwa. Pia amesema kuwa watu
wengine 90 wakiwemo polisi na raia wameuawa.
Usiku kucha
miji ya Ankara na Istanbul ilikumbwa na milio ya risasi na milipuko baada ya
wanajeshi waasi kufanya mashambulizi wakitumia vifaru na helikopta.
Maafisa
wanasema kuwa zaidi ya wanajeshi 1500 wamekamatwa huku wale wa vyeo vya juu
wakiwemo majerali wakipokonywa nyadhifa zao.
ANGALIA SHAMBULIO LAKUTISHA LILILOTOKEA HUKO UFARANSA, BONYEZA HAPA CHINI.
No comments:
Post a Comment