
Baraza la
Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia rasmi wimbo wa ‘pale kati patamu’ ulioimbwa
na Msanii Ney wa Mitengo kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili.
Msanii huyu
amekuwa na tabia na mienendo yenye kuchafua Sekta ya Sanaa yeye binafsi kupitia
kutoa kazi chafu na kufanya maonesho yenye kukiuka maadili. Kazi zake zikikiuka
maadili na kudhalilisha utu wa mwanamke sambamba na kutoa lugha za matusi na za
kudhalilisha watu wa kada mbalimbali.
Ieleweke
kwamba kwa mujibu wa kifungu namba 4(L) cha Sheria ya BASATA namba 23 ya mwaka
1984, Baraza limepewa jukumu la kuhakikisha linalinda maadili miongoni mwa
wasanii wanapokuwa jukwaani au wanapobuni kazi yoyote ya sanaa.
ikumbukwe
kwamba BASATA limeshamuita na kumuonya msanii huyu mara kadhaa kutokana na
tabia yake ya kutoa kazi zisizokuwa na maadili na aliahidi kubadilika na
kuachana na tabia hiyo. Kwa hiyo kuendelea kwake kufanya matukio haya kwa
makusudi ni uthibitisho kwamba hajabadilika na kwa maana hiyo ameendelea
kuidhalilisha Sanaa na wasanii wa kitanzania wenye kujitambua na kuiheshimu
kazi ya sanaa kama kazi nyingine. Kwa sasa Msanii huyu ametoa wimbo mwingine wa
Pale Kati patamu ambao uko mitandaoni ukipambwa na picha chafu zinazoonesha
mwanamke akiwa mtupu yaani uchi wa mnyama.
Kwa mantiki
hii BASATA halitavumilia wasanii wachache ambao wanataka kuigeuza tasnia ya
sanaa na wasanii genge la wahuni wasio na staha na wanaojipanga kuibomoa jamii.
BASATA linapenda kueleza ya kufuatayo · BASATA linatamka kuwa limeufungia wimbo
huu rasmi kutumika kwa namna yoyote ile. · Aidha pamoja na adhabu ya kufungia
wimbo huu hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Aidha,
BASATA linawataka Wasanii wote nchini kufuata sheria, kanuni na taratibu mara
wanapotengeneza kazi zao.
SANAA NI
KAZI, TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI
Godfrey
Mngereza
KATIBU
MTENDAJI
KAMA ULIPITWA NA ILE STORI KALI KUHUSU MUZIKI MPYA WA DIAMOND , NIMEKUSOGEZEA, >>> BONYEZA HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment