Mbwana
Samatta leo anatarajiwa kuonekana tena katika nyasi za Ulaya pale timu yake ya
Genk itakapovaana na KV Oostende katika muendelezo wa mechi za ufunguzi katika
Ligi Kuu ya Ubelgiji maarufu kama Jupiler Pro League.
Mchezo ambao
utachezwa kunako dimba la Cristal Arena, nyumbani kwa Genk utaanza saa 1 kamili
za usiku kwa majira ya Tanzania na Afrika Afrika Mashariki kwa ujumla.
Ikumbukwe
tu, huu ndio msimu ambao Samatta anaanza kuanzia mwanzo mara baada ya msimu
uliopita kuukuta mwishoni kufuatia ksajiliwa katika dirisha dogo akitokea TP
Mazembe ya DRC.
Samatta,
akiwa kama miongoni mwa washambuliaji tegemezi tayari alibainisha dhamira yake
tangu mwanzo kwamba anataka kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao, hivyo ni
jukumu lake sasa kuhakikisha msimu huu timu yake inafanya vizuri ili
kukamilisha ndoto zake.
Msimu
uliopita, Samatta aliwafunga Oostende katika mchezo wa raundi ya pili ya ligi
waliyokutana, hivyo kumbukumbu hii ni morali tosha ya kuhakikisha anaisaidia
tena timu yake kuibuka na ushindi leo.
Genk na
Oostende wamekutana mara kumi katika michuano tofauti-tofauti. Oostende
anaonekana kuwa na rekodi nzuri zaidi baada ya kufanikiwa kushinda michezo 4,
huku Genk wakishinda mara 3 na kutoka sare mara tatu.
Msimu
uliopita Genk walimaliza nafasi ya tano baada ya kujikusanyia alama 48 huku
Oostende wakimaliza nafasi ya nne baada ya kupata alama 49.
No comments:
Post a Comment