Msanii na
mwanamitindo Jokate Mwegelo amefunguka na kumwaga sifa za kutosha kwa msanii
Alikiba na kusema kuwa ni msanii huyo ni mfalme ila hana mbwembwe kama wasanii
wengine.
Jokate
alitumia ukurasa wake wa Instagram kumwaga sifa hizo na kudai kuwa akiwa
amenuna akisikia sauti ya Alikiba anajikuta anafurahi kwani anavutiwa sana na
sauti hiyo.
“Alikiba ni
King wa kutoa ngoma baada ya ngoma, King asiye kuwa na mbwembwe, ni mzuri
kuliko wote, ni mfalme wa sauti ya kumtoa nyoka pangoni. Nikinuna najikuta
nafurahi nikisikia sauti yake, hapa nimesikiliza ‘Nisamehe’ nairudia tu,
Nisamehe ni wimbo wa taifa unakuja kwa kasi ya ajabu”. Aliandika Jokate
Alikiba na
Baraka the Prince wanategemea kuachia wimbo ambao utaiwa ‘Nisamehe’ ni wimbo wa
Baraka the Prince ameshirikisha Alikiba
ANGALIA HII GARI ILIYOTENGENEZWA KWA TEKNOLOJIA YA HALI YA JUU ZAIDI, BONYEZA HAPA CHINI KUONA VIDEO!
No comments:
Post a Comment