
Wakati jeshi
la polisi likisema linajiimarisha, vitendo vya ujambazi vinazidi kuitikisa nchi
baada ya kundi la watu wasiojulikana kuvamia ofisi za Kampuni ya Ahsante Tours
ya mjini Moshi, kuua walinzi wawili na kuiba Sh 65.5milioni.
Tukio hilo
limekuja siku chache baada ya watu wasiojulikana kuvunja duka la kubadilisha
fedha la Chase Forex Bureau De Change la mjini Moshi na kuiba zaidi ya Sh120
milioni.
MTOTO WA DIAMOND TIFFAH PLATNUMZ AANZAKUONYESHA VIPAJI VYA AJABU KUONA ==> BONYEZA HAPA
Mbali na
tukio hilo, Juni 12 mwaka huu, watu watano wakiwa na bunduki aina ya SMG,
walivamia mji wa Magugu wilayani Babati mkoani Manyara na kupora Sh2.5 milioni.
Tofauti na
tukio hilo la Magugu, hivi karibuni Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam
waliwaua watu watatu eneo la Masaki katika majibizano ya risasi na Polisi.
Ukiachilia
matukio hayo, taarifa kutoka mikoa mbalimbali nchini zinaonyesha uporaji wa
fedha na mali kwa kutumia pikipiki maarufu kama bodaboda, unazidi kushika kasi
maeneo mbalimbali.
Wengi wa
wanaolengwa na wahalifu hao ni wateja wanaotoka kuchukua pesa benki au
wanaokwenda kuchukua fedha jambo ambalo limezua hofu kuwa huenda baadhi ya
wafanyakazi wa benki wanashirikiana na wahalifu.
Lakini,
tishio kubwa zaidi la uhalifu linatokana na kuibuka kwa makundi ya kihalifu
yanayokuwa yamejihami kwa silaha za kivita, yakiwamo mabomu ya kurushwa kwa
mkono, yakichinja raia na kupora.
Hivi
karibuni, Polisi Jijini Dar es Salaam waliwaua watuhumiwa hatari wawili
waliokuwa wamejihami kwa bunduki na mabomu, wanaotuhumiwa kuchinja watu nane
Jijini Tanga na watatu Jijini Mwanza
Hali hii
ndio imemsukuma Rais John Pombe Magufuli, kuwaagiza polisi kuhakikisha
‘wanawanyang’anya’ majambazi silaha haraka kabla ya kuwadhuru polisi ama raia
wasio na hatia.
Uporaji
Ahsante Tours
>>>Tukio la
mauaji ya walinzi wawili ofisi za Ahsante Tours, lilitokea usiku wa kuamkia
jana, baada ya watu hao kuwazidi nguvu walinzi na kuwafunga kamba kisha
kuwapiga kwa kitu butu kichwani.
Kampuni hiyo
inamilikiwa na mfanyabiashara Cathbert Swai na mkewe Stella Shangali, ambao pia
wanamiliki hoteli ya kitalii ya Weruweru River Lodge iliyopo Mailisita, nje
kidogo ya mji wa Moshi.
Taarifa
kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo ambayo ni moja kati ya kampuni
zinazoongoza kwa kupokea watalii wengi, zinadai huenda tukio hilo ni mpango wa
ndani.
“Kuna maswali mengi tunajiuliza. Walijuaje
kuna kiasi hicho kikubwa cha fedha kama taarifa hazikutoka miongoni mwetu?”
alihoji mmoja wa wafanyakazi aliyeomba jina lake lisitajwe.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa, alisema kati ya fedha
zilizoibwa, kulikuwa na Dola za Marekani
(Sh50 milioni) na Sh15 milioni za Tanzania.
Walinzi waliouawa wametajwa kuwa ni Omar
Mohamed (48), mkazi wa Matindigani Pasua na Dominick Cheddy (41), mkazi wa
Mailisita na wote ni wenyeji wa mkoa wa Tanga.
Kamanda
Mutafungwa alisema tukio hilo liligunduliwa saa 1.00 asubuhi na wasamaria wema
waliotoa taarifa polisi, na uchunguzi wa awali umebaini watu hao walikata uzio
wa ofisi hizo.
“Baada ya
kuingia ndani ya jengo hilo la ofisi walivunja ofisi ya meneja mkuu na baadaye
ofisi ya mhasibu ndio wakaiba Dola 23,300 na pesa za Tanzania Sh15
milioni,”alisema Kamanda Mutafungwa.
“Tunashuku
kuwa huenda hao majambazi waliamua kuwaua hao walinzi baada ya hao walinzi
kuwatambua. Bahati mbaya hawakuwa na silaha yoyote hata panga hawakuwa
nalo,”alisisitiza.
Kamanda
Mutafungwa alisema Polisi inamshikilia mtu mmoja ambaye inaonekana alikuwepo
wakati mauaji na uporaji huo ukifanyika lakini, majambazi hao hawakumdhuru
sehemu yoyote.
Hata hivyo,
Kamanda Mutafungwa, aliwataka wafanyabiashara kupeleka pesa benki badala ya
kuzihifadhi ndani au ofisini na kuwataka pia kuimarisha ulinzi ikiwamo kuweka
CCCTV Camera.
Alitoa wito
kwa wananchi wenye taarifa za waliohusika na tukio hilo, kulisaidia Jeshi la
Polisi kama ilivyotokea wiki moja iliyopita ambapo taarifa zao zilisaidia
kuwatia mbaroni wahalifu mbalimbali 30.
www.boazmwakasege8.com
ReplyDeletewww.boazmwakasege.com
ReplyDeletewww.boazmwakasege.com
ReplyDelete