
Askari wa
Kikosi cha Usalama Barabarani, Sajenti Mensah wa Kituo cha Polisi Oysterbay
ameuawa usiku huu kwa kupigwa risasi akiwa kazini eneo la Sayansi Kijitonyama
jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Christopher Fuime amesema tukio hilo
lilitokea majira ya saa mbili usiku huu na chanzo cha mauaji hayo
hakijafahamika.
“Tukipata
chanzo itakuwa tayari upelelezi wetu umetimia, hivyo kwa sasa tunalifanyia kazi
ili kubaini wahusika wa mauaji hayo,” amesema
R.I.P KUNDAMBANDA
R.I.P KUNDAMBANDA
No comments:
Post a Comment