
Mkazi mmoja
mkoani Singida anayedaiwa kuwa daktari feki anatuhumiwa kusababisha kifo cha
mgonjwa, Israel Shabani (68) baada ya kumfanyia upasuaji wa tezi dume.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea
Alhamisi iliyopita saa mbili usiku nyumbani kwa mtuhumiwa baada ya kumfanyia
Shabani upasuaji.
Alisema
mtuhumiwa huyo anadaiwa alikuwa akifanya kazi katika vituo vya afya serikalini,
lakini baada ya kuacha alijiita daktari na kuamua kutoa tiba ikiwamo ya upasuaji
nyumbani kwake kinyume na sheria.
Baada ya
kumfanyia upasuaji huo wa kienyeji, mgonjwa huyo alitokwa damu nyingi na kuwa
katika hali mbaya.Mtuhumiwa alipobaini hali hiyo, alimtelekeza na kukimbilia
kusikojulikana.
Alidai kuwa
baada ya polisi kufanya upekuzi kwenye nyumba ya mtuhumiwa huyo, walikamata
vifaa vingi vya tiba zikiwamo dawa za kutibu binadamu.
HAYA NDIO MAKUBALIANO YALIYOFIKIWA NA CLUB YA BAYERN MUNICH, JUU YA #MARIO GOTZE KWENDA BORUSSIA DORTMUND SOMA HAPA CHINI.
No comments:
Post a Comment