
Jana
wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa
Mtandao wa
Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.
Dar/Dodoma.
Sakata Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) limezidi kupanuka baada ya wanafunzi
waliorudishwa nyumbani kupinga kuitwa vilaza.
Jana
wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa
Mtandao wa
Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.
Akizungumza
kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Gibson Johnson alisema wanasikitika kuona
wanavyozushiwa tuhuma mbalimbali kuhusiana na wao kujiunga na chuo hicho.
Alisema
wamekuwa wakijiuliza sababu za Serikali zinazotaka kuhalalisha kutimuliwa kwao
chuoni kuwa hawakuwa na sifa, jambo ambalo si la kweli.
“Siyo kweli
kwamba sisi ni vilaza (wanafunzi wasiofanya vizuri darasani) na waliofeli na
kupata daraja sifuri.
“Sisi ni
wanafunzi tuliofaulu kwa viwango vilivyohitajika kwa daraja la kwanza hadi la
tatu na tulipangiwa shule za kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita,
lakini tulibadili na kuamua kujiunga Udom, hivyo tunaomba Serikali itumie
busara zake.
“Hatuwezi
kwenda kusoma kidato cha tano na sita kwa kuwa tumepoteza muda wetu.”
Alisema
wanamshauri Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako na Rais John Magufuli
kutumia busara kuwarudisha chuoni kumalizia masomo yao.
Katibu Mkuu
wa TSNP, Alphonce Lusako aliitaka Serikali ichukukue hatua kwa waliohusika
kudahili wanafunzi wasio na vigezo na kuwawajibisha.
“Lakini pia
wanafunzi wafidiwe fedha na muda waliopoteza kwa wakati wote waliokuwa chuoni,
kama hawatapewa haki zao, sisi tutashirikiana na wadau wa elimu zikiwamo asasi
za utetezi wa kisheria kutafuta haki mahakama,” alisema Lusako.
Udom
yazungumza
Ofisa
uhusiano wa Udom, Beatrice Baltazali alisema wanafunzi hao wote walifaulu
vizuri wakiwa na daraja la kwanza, pili na wachache daraja la tatu.
“Wanafunzi
wote walikuwa na nafasi ya kwenda kidato cha tano, lakini kwa kuwa waliahidiwa
ajira, waliona wapitie huku kwa kuwa watapata ajira ya moja kwa moja,” alisema.
Beatrice
alisema walimu wa Udom walikuwa wanalipwa fedha za ziada kuwafundisha wanafunzi
wa programu hiyo kwa kuwa walikuwa wanatumia muda mwingi zaidi ya kiwango
walichokuwa wamepangiwa.
“Kutokana na
madai ya malipo hayo, mkaguzi wa ndani aligundua kuna tatizo, ndiyo walimu nao
wakaamua kugoma, wanafunzi wakawa hawafundishwi Serikali ikaamua warudishwe
nyumbani,” alisema Beatrice.
My take; mh
raisi tuelewe lipi na aliangalia wapi mpaka ukajilizisha hawa wanafunzi
kufukuzwa ndani ya masaa 24?
No comments:
Post a Comment