
TAARIFA KWA
UMMA
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Dkt.
Alex L. Kyaruzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO).
Kufuatia
uteuzi huo, Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter M. Muhongo (Mb.),
amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO kuanzia
tarehe 31/5/2016 hadi tarehe 30/5/2019;
1. Dkt. Samwel Nyantahe
2. Dkt. Lugano Wilson
3. Bw. David Elias Alal
4. Mhandisi Stephen Peter Mabada
5. Mhandisi Leonard R. Masanja
Aidha,
Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (Mb) amekamilisha
uteuzi wa Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), kuanzia
tarehe 30/5/2016 hadi 29/5/2019 wajumbe
hao ni :
Bw. Abdalah H. Musa
Dkt. Coretha Komba
Bw. Felix M. Maagi
Dkt.
Lightness Mnzava
Bw. John B. Seka
Uzinduzi wa
Bodi hizo utafanyika Makao Makuu ya Mashiriki hayo Siku ya Alhamisi tarehe 2
Juni, 2016, saa 4:00 asubuhi kwa Bodi ya STAMICO na saa 8:00 mchana kwa Bodi ya
TANESCO.
Imetolewa
na;
KATIBU MKUU
31 MEI, 2016
No comments:
Post a Comment