-
MAELEZO,Dodoma.
Serikali
kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imetenga shilingi bilioni
10 katika mwaka wa fedha 2016/2017 kwa ajili ya ukarabati wa Uwanja wa Ndege wa
Mtwara.
Hayo
yamebainishwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin
Ngonyani leo Bungeni Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Mtwara Vijijini
Mhe. Hawa Ghasia lililohoji kuhusu ukarabati wa Uwanja wa Ndege wa Mtwara.
Mhe.
Ngonyani alisema kuwa Serikali imeendelea kufanya matengenezo ya mara kwa mara
katika uwanja huo na TAA inafanya tathmini ya uchakavu wa matabaka ya lami (Pavement
Evaluation) ya njia ya kuruka na kutua ndege ili kubaini ukarabati stahiki
unaotakiwa na matumizi ya fedha zinazohitajika na kazi hiyo ya tathmini
inatarajiwa kukamilika ifikapo Juni 2016.
Aidha, Mhe.
Ngonyani alieleza kuwa katika mpango wa muda mrefu, Serikali kupitia Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege inaandaa Mpango Kabambe (Master Plan & Concept Design)
kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa uwanja huo kutoka daraja 3C la sasa kwenda
daraja la 4E ili kuweza kuhudumia ndege kubwa zaidi hivyo kuwa kitovu cha
usafiri wa anga kwa Ukanda wa Kusini.
“Ukarabati
na upanuzi wa uwanja utahusisha miundombinu yote ya kiwanja ikiwemo taa na
mitambo ya kuongozea ndege pamoja na majengo. Kazi hiyo ya uandaaji wa Mpango
Kabambe na Usanifu wa Awali inatarajiwa kukamilika Julai 2016.” Alisema
Ngonyani
Ikiwa ni
mpango wa muda mfupi, Mhe. Ngonyani aliongeza kuwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
imeingia makubaliano na Kampuni ya British Gas (BG) kwa ajili ya kutumia taa
zake ambazo ni za kuhamisha kwa ajili ya kuongozea ndege pale ambapo ndege
itatakiwa kutua usiku katika uwanja huo.
No comments:
Post a Comment