
Ndoa nyingi
zinaingia kwenye migogoro kwa sababu ya mambo ya kukurupuka na kufanya haraka
bila wahusika kufahamiana vizuri, hebu tuzingatie yafuatayo ili tusiseme
'NINGEJUA NISINGEOA/NISINGEOLEWA'
1. Chanzo
cha uhusiano wenu kiwe ni upendo wa dhati
2. Chunguza
kwa mwenzio juu ya tabia:nidhamu, adabu, hasira, ulevi na umalaya
3. Mpeane
muda wa kutosha kufahamiana
4. Mtembee
pamoja maeneo tofautitofauti kama michezoni, bar na out mbalimbali ili muone
interest za kila mmoja
5. Muwe wa
imani moja. ila kama mmeshibana sana na mwaweza kuvumiliana hata wa imani
tofauti ni sawa.
6. Wajue
ndugu wa mwenzio ili kupata habari zao zitakazokufahamisha mwenzao pia yukoje
7. Pimeni
afya zenu bila aibu. kuna maradhi mengi kama HIV/AIDS na mengine.
8. Kama ni
Mkristo au Muislam funga ndoa Kanisani au Msikitini na siyo Bomani.
9.Kwa
Wakristo ndoa haina talaka. huu ni mpango wa Mungu. kuachana na kuoa mwingine
ni dhambi.
No comments:
Post a Comment