Mahakama Kuu
ya Mkoa wa Mwanza imetengua kifungo kwa mzazi mwenzake na Nay Wamitego, Siwema
kwa kumhukumu kifungo cha nje cha miaka miwili.
Siwema-akilia-kwa-uchungu-baada-ya-kuona-nyumba-mpya-ya-mume-wake
Mwezi April
mahakama kuu ya Mkoa wa Mwanza ilimhukumu Siwema kifungo cha miaka miwili jela
baada ya kukutwa na kesi kumtukana matusi kwa njia ya mtandao mlalamikaji
ambaye anafahamika kwa jina la Deo.
Nay Wamitego
amesema, “Ndiyo ana kifungo cha nje, nimemsaidia kama mzazi mwenzangu sijawahi
kufikiria kurudiana naye. Nimefight mimi na ndugu zake ilimradi nitimiza kile
ambacho niliwaahidi watu kile ambacho nilizungumza.”
Aidha Nay wa
Mitego ameongeza kuwa ameonana na mzazi mwenzake huyo siku ya mwisho tangu
amefungwa na wala hana mawasiliano naye tena kwa kukwepa kuanzisha mambo
mengine yasiyokuwa na msingi.
No comments:
Post a Comment