Ajali
zimeendelea kutokea katika barabara za mabasi yaendayo haraka ambazo zimekuwa
zikisababishwa na madereva wasiotaka kufuata sheria za barabarani ambapo leo
katika mataa ya kuongozea magari Shekilango basi moja liendalo haraka
limegongana na pikipiki.
Ajali hiyo
ambayo haikusababisha vifo wala majeruhi imetokea majira ya saa sita ambapo kwa
mujibu wa mashududa dereva wa boda boda akiwa na abiria mwanamke alikuwa
akikatiza kwenye taa hizo akitokea upande wa soko la shekilango akielekea
milleniam park huku taa zikiwa zimeruhusu basi hilo kupita na kusababisha
kugongana na pikipiki kupinduka.
Askari wa
usalama wakiwa katika harakati za kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo akatokea
dereva
mwingine wa
bodaboda kukatiza katika eneo hilo bila kufuata sheria ambaye nae alikamatwa na
kuambatanishwa na waliosababisha ajali hiyo na kupelekwa kwenye vyombo vya dola
kwa hatua zaidi.
No comments:
Post a Comment