
Brazil inatajwa kuwa nchi ya nne duniani kwa kuwa na idadi
kubwa ya Wafungwa gerezani ambapo ina Wafungwa 600,000 kwenye magereza yake na
kama unakumbuka hivi karibuni kumekuwa na matukio ya kihalifu ndani ya Magereza
na yamesababisha vifo vya wafungwa 140.
Sasa kingine kilichoripotiwa ni kutokea kwenye gereza la
Franco da Rocha ambapo Njiwa amekamatwa na Askari akipeleka simu ya mkononi kwa
mfungwa ambapo bado haijafahamika aliyekuwa akimtumia Ndege huyo kupeleka simu.
Kuna maswali mengi ya kujiuliza lakini hayajajibiwa…. Njiwa
huyo alielekezwa vipi? akili gani imetumika kumuongoza? alikua anatumia njia
gani kuikabidhi simu?


No comments:
Post a Comment