
Mtu mmoja
amefariki dunia kwa kukatwa kichwa na kiwiliwili chake kutelekezwa kichakani
katika Kijiji cha Rushwa, Kata ya Mushabago, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera.
Mwenyekiti
wa Kitongoji cha Buyango, Gasper Joseph amesema wamelazimika kuita wananchi ili
kuutambua mwili wa marehemu.
Amesema
licha ya kiwiliwili kutelekezwa kwenye eneo la kichaka, kichwa cha marehemu
huyo wa kiume hakikuwapo kwenye eneo hilo jambo ambalo alilosema limeleta hofu
kwa wananchi.
“Nimeita
watu na walikusanyika, hata hivyo walishindwa kuubaini mwili huo kwa kuwa
kichwa chake hakikuonekana. Mwenyekiti wa Kijiji cha Rushwa alitoa taarifa
polisi kwa ajili ya hatua zaidi ili turuhusiwe kuzika,” amesema Joseph.
HAYA NI MAAJABU MAPYA MTOTO KAONYESHA KUIPENDA BIA ZAIDI KULIKO MAZIWA, TAZAMA VIDEO HAPA CHINI, PIA SUBSCRIBE KUPATA VIDEO ZAIDI!
No comments:
Post a Comment